Duru mpya ya mzozo iliyozushwa na Ufilipino ina lengo gani?
2024-03-28 10:50:35| cri

Hivi karibuni Ufilipino imezusha mzozo mara kwa mara katika Bahari ya Kusini ya China, ikiwa ni pamoja na kutuma meli kuingia kiharamu katika eneo la bahari karibu na Ren’ai Jiao (Second Thomas Reef), na kutoa vifaa vya ujenzi na huduma nyingine kwa meli ya kijeshi iliyojidai kuwa imekwama kwenye eneo hilo ambayo ni hatua inayokwenda kinyume cha sheria, na kujaribu kujenga vituo vya kudumu kwenye visiwa visivyo na makazi. Lakini njama hiyo ya Ufilipino ilishindwa kutokana na hatua halali za polisi wa bahari wa China. Je, Ufilipino inafanya hivyo kwa malengo gani?

Wachambuzi wanaona hatua hizo za Ufilipino zina malengo matatu. Kwanza, inajaribu kuzusha mzozo na kuchafua taswira ya China katika jumuiya ya kimataifa, ili kuimarisha madai haramu ya Ufilipino dhidi ya Bahari ya Kusini ya China. Pili, inajaribu kuchochea mvutano kuhusu suala la Bahari Kusini, ili kutoa kisingizio kwa Marekani kuingilia kati masuala ya kikanda. Ufilipino ikiwa mfuasi wa Marekani inatoa misaada kadiri iwezavyo kwa uwepo wa Marekani katika kanda ya Asia-Pasifiki, huku suala la Bahari Kusini likiwa ni kisingizio kizuri. Aidha, Marekani, Japan na Ufilipino zitafanya mkutano wa kilele mwezi Aprili huko Washington, ambapo suala la Bahari ya Kusini ya China linatazamiwa kufuatiliwa zaidi.

Baadhi ya watu nchini Ufilipino pia wamedai mara kwa mara kwamba, watawasilisha mamlaka ya utawala ya China katika Bahari ya Kusini kwa usuluhishi wa kimataifa. Kama tujuavyo, mamlaka ya utawala ya China kwa ardhi na baharini zilipatikana na kuthibitishwa katika mchakato wenye historia ndefu, ambayo yana ushahidi na msingi wa kutosha wa kihistoria na kisheria, na kulingana na sheria za kimataifa kama vile Katiba ya Umoja wa Mataifa, na Mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya Sheria ya Bahari. Eneo la ardhi la Ufilipino linafafanuliwa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa ambalo siku zote halijumuishi kisiwa au mwamba wowote wa Visiwa vya Nansha. Ufilipino kutuma mara kwa mara meli kuingia kiharamu kwenye eneo la bahari la China, kumekiuka vibaya mamlaka ya ukamilifu wa ardhi na haki na maslahi za bahari za China.

Balozi wa Marekani nchini Ufilipino MaryKay Loss Carlson alipohojiwa na vyombo vya habari nchini Ufilipino amesema, mkataba wa ulinzi wa pamoja kati ya Marekani na Ufilipino una “thamani kubwa” katika kuzuia migogoro katika eneo hilo. Sasa watu wanataka kuuliza kuwa, chini ya uchochezi wa Marekani, Ufilipino unazusha migogoro mara kwa mara na kuharibu amani na utulivu wa kikanda, zitatoa mchango na thamani gani kwa utaratibu wa kikanda? Je, muungano wa Marekani na Ufilipino umeleta utulivu au vurugu katika eneo hilo? Ukweli wa mambo umetoa majibu.