Naibu mkuu wa Majeshi nchini Sudan amesema jeshi la nchi hiyo lina uwezo wa kuvishinda vikosi vya RSF
2024-03-28 11:04:54| cri

Mjumbe wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan na Kaimu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan, Shams-Edin Kabashi amesisitiza kuwa, jeshi hilo lina uwezo wa kupata ushindi dhidi ya Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF).

Akizungumza na maofisa na wanajeshi katika Eneo la Kijeshi la Mashariki mkoani Gedaref, mashariki mwa nchi hiyo hapo jana, Kamanda huyo amesema jeshi la Sudan linaungwa mkono na wananchi, na liko katika hali nzuri kwa pande zote, pia amesema jeshi hilo linakaribia kupata ushindi dhidi ya kikosi cha RSF.

Sudan imeshuhudia mapigano makali kati ya Jeshi la nchi hiyo na kikosi cha RSF tangu mwezi April mwaka jana, na kwa mujibu wa makadirio ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, mpaka sasa, watu 13,900 wameuawa tangu kuanza kwa mapigano hayo.