Umoja wa Afrika watoa wito wa kuhakikisha Afrika inajitosheleza kwa chanjo na dawa
2024-03-28 11:05:48| cri

Umoja wa Afrika umesisitiza haja ya kuhakikisha Afrika inajitosheleza katika uzalishaji wa dawa na chanjo.

Kauli hiyo imetolewa na naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Monique Nsanzabaganwa wakati akihutubia Mkutano wa Kimataifa wa uvumbuzi, Hakimiliki ya uvumbuzi na Uhamishaji wa Teknolojia katika Sekta ya Madawa barani Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia tarehe 25 hadi 26 mwezi huu.

Katika taarifa yake, Umoja wa Afrika umesema Bi. Nsanzabaganwa amesema, ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa madawa barani Afrika, Umoja huo umekiwezesha Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kuchukua nafasi ya uongozi katika sekta ya afya ya umma barani humo.

Ametoa wito wa juhudi za pamoja ili kuboresha uvumbuzi, uhamishaji wa teknolojia, na uhusiano wa ufanisi ili kujenga sekta ya madawa inayojitegemea na ya uvumbuzi barani Afrika.