Serikali ya Tanzania kupanua uhuru wa habari
2024-03-28 11:05:20| cri

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema mabadiliko katika Sheria ya Huduma za Habari yamekuja kukuza sekta ya habari kwa kiwango kikubwa.

Majaliwa ameyasema hayo jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Amesema, dhamira ya serikali ni kuendelea kufanya maboresho ya sera ili kuwe na sheria na kanuni rafiki katika kuendesha masuala ya habari nchini humo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema, mageuzi hayo yamewezesha jamii ya Tanzania kupata habari, sekta binafsi kuendesha vyombo vya habari, na kwamba mkakati sasa ni kupanua wigo zaidi wa mifumo ya watu kuanzisha vyombo vya habari.

Kauli ya Majaliwa imekuja ikiwa ni miezi 11 tangu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha mabadiliko ya Sheria ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016, Juni 13, 2023.