China yatoa mwito wa kupunguza mvutano mashariki mwa DRC
2024-03-28 08:59:41| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa balozi Dai Bing jana kwenye baraza la usalama kuhusu suala la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametoa mwito kwa pande husika kufanya kila juhudi kupunguza mvutano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Balozi Dai Bing amesema katika siku za hivi karibuni, migogoro ya kivita imeongezeka mashariki mwa DRC, na matukio ya usalama mipakani yanatokea mara kwa mara, na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya raia na kulazimisha watu wengi kukimbia makwao.

China imelitaka kundi la "M23" na makundi mengine yenye silaha kusimamisha vita mara moja na kuondoka kwenye maeneo yanayokalia, na kuzitaka pande husika kujizuia, kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo, na kufanya juhudi zote kutuliza mvutano kwenye eneo hilo.