Watu 14 wafariki kutokana na kimbunga Gamane nchini Madagascar
2024-03-29 23:08:09| cri

Watu 14 wamefariki, wengine watatu kujeruhiwa na wengine watatu hawajulikani walipo baada ya kimbunga Gamane kuikumba Madagascar.

Idara ya Kudhibiti Hatari na Maafa ya nchini Madagascar (BNGRC) imesema, kimbunga hicho kililikumba eneo la ncha ya kaskazini ya nchi hiyo jumatano asubuhi, kikiambatana na upepo mkali na mvua kubwa.

Idara hiyo imesema, mafuriko yaliyotokana na kimbunga hicho yamesababisha hasara kubwa, ambapo nyumba 6,675 zilisombwa na mafuriko na mashamba 1,698 ya mpunga kufunikwa na maji yaliyotokana na mafuriko hayo, huku nyumba nyingine 617 zikiharibika.