Umeme wakatika nchi nzima Ethiopia
2024-03-29 10:05:23| cri

Shirika la Nishati ya Umeme la nchini Ethiopia (EEP) limesema, umeme umekatika nchi nzima hapo jana kutokana na hitilafu katika mfumo wa uendeshaji.

Shirika hilo limesema, umeme ulikatika nchi nzima kuanzia jana mchana isipokuwa katika Mji wa Bahir Dar na maeneo ya jirani, ambao uko mkoa wa Amhara, kaskazini mwa Ethiopia.

Shirika hilo limesema juhudi zinaendelea kurejesha mfumo wa usambazaji wa umeme, na uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha mfumo huo kushindwa kufanya kazi na kusababisha ukosefu wa umeme nchini humo.