Kenya yazindua hifadhidata ya matokeo ya utafiti
2024-03-29 08:46:17| CRI

Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu Kenya Bibi Beatrice Inyangala, amesema Kenya imezindua hazina ya kitaifa ya matokeo yote ya utafiti unaofanywa nchini Kenya.

Akiongea na wanahabari mjini Nairobi, Bibi Inyangala amesema kanzidata hiyo ina hazina ya ufikiaji iliyo wazi inayolenga kufanya matokeo ya utafiti yapatikane kwa umma kwa uhuru.

Amesema hazina hiyo itakayokuwa kwenye jukwaa la kidijitali, litaongeza usambazaji na ufikiaji wa utafiti na kuhimiza matumizi tena ya data za utafiti ili kuchochea utafiti zaidi.

Ofisa mtendaji mkuu wa Mfuko wa Kitaifa wa Utafiti unaomilikiwa na serikali Bw. Dickson Andala, amesema hazina hiyo inawezesha utayarishaji wa ripoti za uchambuzi ambazo zitatoa ufahamu katika vichocheo vya utafiti, matumizi na biashara ya matokeo ya utafiti.