Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema, watu zaidi ya milioni 1.1 katika ukanda wa Gaza wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, wakati Israel inazuia msaada kuingia katika sehemu hiyo.
Ofisi imetoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii ikisisitiza haja ya kupeleka msaada wa chakula wa kuokoa maisha kupitia njia za ardhini, hasa katika maeneo ya kaskazini ya ukanda huo. Ofisi hiyo imeongeza kuwa vizuizi bado vinakuwepo, na wakati unaenda haraka.
Wakati huohuo vyanzo vya matibabu vimetangaza kifo cha mtoto mmoja katika eneo la Beit Lahia kaskazini ya Gaza kilichotokana na njaa na ukosefu wa tiba, na kufanya idadi ya vifo vya watoto vilivyotokana na utapiamlo kuongezeka hadi kufikia 30.