Bibi Peng Liyuan akutana na walimu na wanafunzi wa Ujerumani mjini Beijing
2024-03-29 08:33:26| CRI

Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan amekutana na ujumbe wa wanafunzi na walimu kutoka Kwaya ya Kichina ya Burg Gymnasium, shule moja ya sekondari ya juu ya Ujerumani, katika shule ya 35 ya sekondari ya juu ya Beijing.

Bibi Peng amepongeza kwaya hii kwa mafanikio yake iliyoyapata katika muongo uliopita ya kueneza urafiki kupitia nyimbo.

Bibi Peng amesema, kupitia juhudi za pamoja za kila mtu, kwaya hiyo imejenga daraja la mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Ujerumani na imekuwa alama inayog’ara ya urafiki kati ya nchi hizo mbili. Ameeleza matumaini yake kuwa wanafunzi wanaweza kujisikia mvuto wa utamaduni wa China kwenye nyimbo, na kuwa mabalozi wa kizazi kipya wa urafiki kati ya China na Ujerumani.