Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na washirika wake Alhamisi wametoa wito wa kupatiwa dola bilioni 1.4 za kimarekani katika mwaka 2024, ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini walioko katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda kupitia mtaji mpya.
Mkurugenzi wa UNHCR kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu Mamadou Dian Balde, amesema katika muongo uliopita, washirika wamepata maendeleo makubwa yanayoonekana kidhahiri. Amesema kama rasilimali ikipatikana, msaada wa kibinadamu wa uwekezaji kwa wakimbizi na jamii utawezesha mpango wa utatuzi wa muda mrefu.