Tovuti ya Kimataifa ya Beijing ya toleo jipya yazinduliwa kwa kuwahudumia wageni na kampuni za kigeni
2024-03-31 14:18:45| CRI

Tovuti ya Kimataifa ya Beijing ya toleo jipya (International Web Portal of Beijing) imezinduliwa hivi karibuni kwa kutoa huduma kamilifu kwenye mtandao wa Internet kwa wageni na kampuni za kigeni walioko Beijing, mji mkuu wa China.

Tovuti hiyo ya toleo jipya inayojumuisha huduma za utoaji wa taarifa, huduma za umma na utoaji wa mashauriano inapatikana kwa lugha tisa zikiwemo Kiingereza, Kikorea, Kijapani, Kijerumani, Kifaransa, Kispania, Kirusi, Kiarabu na Kireno, ikilenga kutoa huduma tele na rahisi kwa watu wa kigeni wakiwemo wawekezaji wageni katika mambo ya malipo, safari, masomo, maisha na utalii.

Kwa mfano, inatoa maelekezo kamili ya huduma kwa kampuni za kigeni kuwekeza na kufanya kazi mjini Beijing, pamoja na maelezo juu ya sera mbalimbali za uwekezaji zilizofuatiliwa nazo. Pia inatoa maelekezo ya huduma zaidi ya 300 zilizo rafiki kwa wageni, na mambo zaidi ya 50 yakiwemo usajili wa malazi, usindikaji wa visa n.k yanaweza kupangwa na kushughulikiwa mtandaoni.