Ujumbe wa Israel waelekea Misri kwa ajili ya mazungumzo ya kusimamisha vita na kuachilia mateka
2024-04-01 09:41:10| CRI

Ujumbe wa maofisa usalama wa Israel umekwenda Misri jana kwa ajili ya mazungumzo ya kuachilia mateka wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kusimamisha vita.

Ujumbe huo unajumuisha wawakilishi wa Shirika la Ujasusi la Israel Mossad, Idara ya usalama wa ndani ya Shin Bet, na wawakilishi kutoka jeshi la nchi hiyo.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema, Waziri Mkuu huyo amezungumza na wakuu wa Mossad na Shin Bet na kuridhia duru inayofuata ya mazungumzo itakayofanyika Doha, Qatar na Cairo, Misri.

Qatar, Misri na Marekani zimekuwa zikipendekeza kubadilishana mateka na kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, ambapo mapigano yalisimamishwa mara ya kwanza kwa wiki moja tu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.