Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) imesema, idadi ya safari za ndege nchini humo itaongezeka taratibu katika majira ya joto na mpukutiko mwaka huu.
Mamlaka hiyo imesema, kuanzia tarehe 31 Machi hadi tarehe 26 Oktoba, mashirika 188 ya ndege ya ndani na nje yanatarajiwa kupanga safari 122,000 za ndege za abiria na mizigo kwa wiki.
Kwa upande wa safari za ndege za kimataifa, safari 17,257 za ndege za abiria na mizigo zitapangwa kila wiki, ambazo zinaunganisha China na nchi nyingine 70, ikiwa ni pamoja na nchi 51 za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.