Serikali mpya ya Palestina yaapishwa
2024-04-01 09:45:06| CRI

Serikali mpya ya Palestina inayoongozwa na Waziri Mkuu Mohammad Mustafa imeapishwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hapo jana.

Serikali hiyo ina mawaziri 23, wakiwemo mawaziri sita kutoka Ukanda wa Gaza, na Waziri Mkuu Mustafa pia anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje.

Uteuzi huo umekuja baada ya serikali ya zamani kujiuzulu kutokana na mazingira magumu yaliyotokea katika Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Jerusalem, pamoja na shinikizo kubwa kwa rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kuifanyia mageuzi serikali na kuanzisha mfumo wa kisiasa wenye uwezo wa kutawala taifa la baadaye la Palestina baada ya kumalizika kwa mgogoro wa Gaza.