Benki ya Kigali yazindua fursa za biashara ya kilimo ili kuwawezesha wajasiriamali wanawake
2024-04-01 23:31:49| cri

Benki ya Kigali (BK) imeanzisha utaratibu maalum uliandaliwa hivi karibuni mahsusi kwa sekta ya biashara ya kilimo, kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanawake na kuwasaidia katika kupanua biashara zao.

Shirikisho la sekta binafsi la Rwanda (PSF) kwa kushirikiana na Benki ya Rwanda wamezindua bidhaa zake mpya za kifedha, kwa ajili ya kuongeza ufahamu kuhusu fursa ndani ya sekta ya biashara ya kilimo. Utaratibu huo unajumuisha machaguo ya fedha kwa kuzingatia wanawake katika mnyororo wa thamani wa biashara ya kilimo, pamoja na masuluhisho ya kifedha kwa wafanyabiashara katika sekta hiyo.

Mkuu wa Idara ya biashara ya kilimo katika Benki ya Kigali Bw. Alexis Bizimana, amesisitiza umuhimu wa dhamira ya Benki ya Kigali katika kuwasaidia wanawake kwenye sekta ya biashara ya kilimo.