Upungufu wa fedha waathiri wajasiriamali wa Afrika, na kusababisha upotevu wa ajira
2024-04-01 10:32:29| cri

Kampuni ndogo 20 zilifungwa kote barani Afrika mwaka jana, na nyingine nyingi zaidi zilipunguza shughuli zao kutokana na ukosefu wa jumla wa fedha ulioathiri nchi nyingi za Afrika, na kusababisha upotevu mkubwa wa ajira.

Mwaka jana, kiasi cha fedha kilichokusanywa na wenye makampuni kama hayo barani Afrika kilipungua kwa asilimia 31 hadi kufikia takriban dola bilioni 4.5, kutoka dola bilioni 6.5 zilizokusanywa mwaka wa 2022, na kuathiri mtiririko wa fedha kwa makampuni hayo.

Kwa mujibu wa jumuiya ya wajasiriamali ya Afrika (AVCA), idadi ya makampuni madogo ambayo hapo awali yaliongeza kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa wawekezaji, mwaka jana yalifungwa baada ya kushindwa kukusanya fedha.

Kwenye ripoti yake ya hivi karibuni AVCA amesema upungufu huu wa fedha umesababisha makampuni kadhaa kupunguza kwa kiasi kikubwa shughuli au kufunga kabisa shughuli zao.