Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema, Judith Tuluka Suminwa ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.
Suminwa ambaye alikuwa Waziri wa Mipango tangu mwezi Machi mwaka jana, ameingia katika historia kama mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini DRC.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuteuliwa, Bi. Suminwa amesema kazi iliyo mbele yake ni ngumu na changamoto ni nyingi, lakini amesema kwa kuungwa mkono na rais wa nchi hiyo pamoja na umma, watafanikiwa kuzikabili.