China kuchukua hatua za majibu endapo Marekani itaweka vizuizi vya visa kwa maofisa kutoka Hong Kong
2024-04-02 09:15:08| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China itacjhukua hatua kali za majibu kama Marekani itaweka vizuizi vya visa kwa maofisa wa Hong Kong.

Wang amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari ikiwa ni majibu ya tangazo la Marekani kuwa inachukua hatua kuweka vizuizi vipya vya visa kwa maofisa wa Hong Kong.

Wang amesema, ripoti hiyo iliyotolewa tena na Marekani mwaka huu, imeshambulia na kuichafua Sheria ya Kulinda Usalama wa Taifa katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, na pia mfumo wa uchaguzi wa Hong Kong na Mpango wa Kulinda Usalama wa Taifa.

Wang amesema, Marekani inapuuza demokrasia ya Hong Kong, utawala wa kisheria, haki za binadamu na uhuru, na kutangaza kuweka vizuizi vipya vya visa kwa maofisa wa Hong Kong, madai ambayo hayana ukweli wowote.