Rais wa China afanya mazungumzo na rais mteule wa Indonesia
2024-04-02 09:16:34| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na rais mteule wa Indonesia, Prabowo Subianto, ambaye yuko ziarani hapa China.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika jana hapa Beijing, rais Xi amempongeza Prabowo kwa kushinda uchaguzi, na kumtaka kupeleka salamu zake za dhati kwa rais wa sasa wa Indonesia, Joko Widodo.

Akizungumza maendeleo na matunda ya uhusiano kati ya pande hizo mbili katika muongo uliopita chini ya viongozi hao wawili, rais Xi amesema China inachukulia uhusiano wake na Indonesia katika mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na iko tayari kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na Indonesia.

Kwa upande wake, rais mteule Prabowo anaunga mkono maendeleo ya uhusiano wa karibu kati ya nchi yake na China, na ataendeleza sera rafiki ya nchi yake kuhusu China.