Rais Paul Kagame wa Rwanda amewataka wanyarwanda kujivunia na kufurahia mafanikio iliyoyapata nchi yao katika miaka 30 iliyopita, tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, akitaka kuwa na nguvu ya msukumo na kusonga mbele kwa kasi.
Rais Kagame amesema hayo jana akizungumza na vyombo vya habari vya ndani. Majadiliano hayo yaligusia mada tofauti ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ijayo ya miaka 30 ya Mauaji ya Kimbari pamoja na safari ya mabadiliko ya Rwanda katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.
Wanyarwanda na marafiki wa Rwanda, Aprili 7, wataanza shughuli za wiki nzima kukumbuka mauaji ya kimbari ya 1994 yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu milioni moja katika siku 100.