Marais wa China na Marekani wafanya mazungumzo kwa njia ya simu
2024-04-03 09:23:43| CRI

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani Joe Biden, ambapo viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili.

Rais Xi amesisitiza kuwa suala na mtazamo wa kimkakati ni msingi muhimu wa uhusiano kati ya China na Marekani. Amesema nchi hizo mbili hazitakiwi kuvunja uhusiano wao ama kuingia katika vurugu na mvutano, bali zinapaswa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa masikilizano kwa Amani na kutafuta ushirikiano wa kunufaishana. Rais Xi amesisitiza kanuni tatu zinazopaswa kuongoza uhusiano kati ya China na Marekani kwa mwaka huu, ambazo ni kuthamini amani, kutoa kipaumbele kwenye utulivu, na kudumisha uaminifu. Amesema suala la Taiwan ni mstari ambao haupaswi kuvukwa katika uhusiano kati ya China na Marekani, na kuweka msimamo wa China katika masuala mengine ikiwemo yanayohusiana na Hong Kong, haki za binadamu, na Bahari ya Kusini ya China.

Kwa upande wake, rais Biden amesema Marekani haitaki kuanzisha Vita mpya ya Baridi, na haitaki wenzi wake kuwa na mvutano na China. Amesema Marekani inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja na haina lengo la kuzuia maendeleo ya China.