Vituo vya mpakani mwa Kenya na Somalia vitaendelea kufungwa huku vikosi vya Umoja wa Afrika ATMIS vikiendelea kupunguzwa. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Kenya Bw. Raymond Omollo amesema hatua hiyo inatokana na haja ya kulinda usalama wa nchi katika maeneo yote ya kuingia na kutoka. Kauli ya Dkt Omollo inakuja miezi tisa baada ya bosi wake Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki, na mwenzake wa Somalia Mohamed Ahmed Sheikh Ali kutangaza nia yao ya kufungua tena mpaka baada ya mashauriano ya ngazi ya juu yaliyofanyika Nairobi, ambayo yangemaliza kizuizi cha miaka 12 kilichoanza mwaka wa 2011. Kenya ina mpaka wa takriban kilomita 800 na Somalia, Dk Omollo amesema kumekuwa na changamoto ngumu sana kupata usalama kwenye mpaka huo.