Watu 10 wameuawa katika shambulizi lililofanywa Jumanne jioni na waasi wa kundi la ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa mujibu wa mshirika ya kiraia ya eneo hilo, waasi wa ADF walivamia kijiji cha Mangodomu kilichoko eneo la Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambacho kimekuwa chini ya utawala wa kijeshi na polisi kuanzia mwaka 2021.
Msimamizi wa eneo la Beni Kanali Charles Omeonga amewahakikishia wakazi nia thabiti ya jeshi la DRC kuwaondoa waasi wa ADF.