Kenya yaanzisha agenda ya sera ya kuhimiza mchakato wa utandawazi wa viwanda
2024-04-04 09:03:38| CRI

Kenya Jumatano imeanzisha Agenda ya 2024 ya kutoa kipaumbele katika sekta ya utengenezaji, ili kuhimiza mchakato wa utandawazi wa viwanda nchini humo.

Katibu mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda nchini humo Bw. Juma Mukhwana amesema, agenda hiyo ya sekta ya utengenezaji yenye vipaumbele vinne inaweka mpango wa kuongeza mchango wa sekta ya utengenezaji kwenye pato la taifa kutoka asilimia 7.8 hadi asilimia 20 itakapofika mwaka 2030.

Ameongeza kuwa, moja ya mambo makuu kwenye agenda hiyo ni kutetea upatikanaji wa umeme na mafuta kwa bei nafuu, mambo yanayoathiri nguvu ya ushindani katika sekta ya utengenezaji. Pia amesema, agenda hiyo inatilia maanani matumizi ya sekta ya viwanda vya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi kupitia kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo zinazouzwa nje ya nchi.