Rais wa China atoa wito wa kuongeza juhudi za upandaji miti kote nchini
2024-04-04 08:58:44| CRI

Rais Xi Jinping wa China tarehe 3  alishiriki kwenye shughuli ya kupanda miti kwa hiari iliyofanyika katika bustani ya misitu iliyopo  eneo la Tongzhou hapa Beijing, na kutoa wito wa juhudi za nchi nzima katika upandaji wa miti ili kujenga China ya kupendeza .

Rais Xi amesema, shughuli ya kupanda miti inalenga kutoa wito kwa watu wote kuchukua hatua za kivitendo na kushiriki katika upandaji wa miti na juhudi za kuongeza misitu ili kuongeza mwonekano wa kijani katika ujenzi wa China ya kupendeza.

Rais Xi  na viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu wa China Li Qiang, waliwasili katika eneo hilo mapema asubuhi na kushirikiana na wakazi wa eneo hilo kupanda miti.