SGR ya Tanzania yaendelea kupokea mabehewa ya kisasa
2024-04-04 11:03:04| Cri

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuwasili kwa mabehewa ya treni za kwanza ya (EMU) katika bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni hatua kubwa ya kusonga mbele kwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) wa Tanzania. Mabehewa ya awali yanajumuisha injini tano za umeme na mabehewa matatu ya abiria.

Injini na mabehewa haya yamenunuliwa nchini Korea Kusini, yaliyotengenezwa kuwa na mazingira ya anasa na urahisi. Kila treni inaweza kubeba hadi abiria 589, na kwenda kwa kasi ya hadi kilomita 160 kwa saa. Mabehewa yatakuwa na huduma kama vile Wi-Fi, viti maalum kwa abiria wenye mahitaji maalum, viyoyozi, na kamera za CCTV kwa usalama.