Tanzania yatajwa kuwa ya pili barani Afrika kwa usalama wa taarifa binafsi
2024-04-04 11:03:59| Cri

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Bw. Nape Nnauye, amesema Tanzania imekuwa ya pili barani Afrika kwa usalama wa taarifa binafsi. Bwana Nnauye ameeleza hayo akinukuu taarifa ya Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano la (ITU) kwa kusaidiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Usalama Mtandaoni ‘the Global Cybersecurity Index’ kwenye uzinduzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) uliofanyika mjini Dar es Salaam.

Amesema, uwepo wa sheria tatu muhimu zinazosimamia usalama mtandaoni, yaani; Sheria za Makosa ya Mtandao 2015, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki 2015 na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi ya mwaka 2022 na uwepo wa taasisi imara kama TCRA na sasa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ni moja ya vigezo vilivyofanya Tanzania kuwa ya pili kwa usalama Mtandaoni katika bara la Afrika.