Mtaalamu wa Uingereza: China ina Mamlaka ya visiwa vya Bahari ya Kusini
2024-04-04 11:09:18| Cri

Hivi karibuni, Anthony Carty, mwandishi wa Kitabu cha “Historia na Mamlaka ya Bahari ya Kusini” ambaye pia ni mtaalamu wa sheria za kimataifa wa Uingereza, amesema visiwa vya Bahari ya Kusini ni sehemu isiyotengeka ya ardhi za China tangu enzi ya kale, na kwamba mamlaka ya China kwa visiwa vya Bahari ya Kusini ina msingi wa kutosha wa kihistoria na kisheria. 

Bw. Carty alipojulisha hatua yake ya kuandika kitabu hicho alisema, baada ya juhudi za zaidi ya miaka 10, amesoma nyaraka za kitaifa za Ufaransa, Uingereza na Marekani kuhusu mamlaka ya visiwa vya Bahari ya Kusini tangu mwishoni mwa karne ya 19, na kufanya ukaguzi halisi, alifafanua mabadiliko ya kihistoria ya visiwa vya Bahari ya Kusini na kuthibitisha kuwa mamlaka ya visiwa vya Bahari ya Kusini inamilikiwa na China, na kutoa nyaraka muhimu za kihistoria na ushahidi wa kimataifa kwa utafiti wa mamlaka ya visiwa vya Bahari ya Kusini.