Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ya Tanzania yakamata shehena kubwa ya bangi mpakani
2024-04-05 09:55:45| Cri


 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) imesema imekamata kiasi kikubwa cha bangi iliyoboreshwa katika mpaka wa Zambia na Tanzania.

Kamishna Mkuu wa DCEA, Aretas James Lyimo, amesema dawa zilizonaswa zinazojulikana kwa jina la 'Skanka' zilifichwa kama bidhaa zisizo na madhara, zinazofanana na majani ya chai au vitafunwa, na zilitoka nchi za Kusini mwa Afrika (Eswatini, Malawi, Zambia, na Afrika Kusini)

Tofauti na bangi inayolimwa nchini Tanzania, bangi iliyokamatwa imeimarishwa kwa kemikali iliyokamatwa kwenye mpaka iliongezwa nguvu kwa asilimia 40, na kuifanya kuwa na nguvu mara nne zaidi.