Majopo ya washauri bingwa nchini Zambia yaunga mkono pendekezo la China la jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja
2024-04-05 09:49:43| CRI

Ubalozi wa China nchini Zambia umeandaa warsha yenye lengo la kutambulisha na kujadili pendekezo la China la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ili kuongeza uelewa wa sera ya mambo ya nje ya China kwa wasomi wa Zambia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti iliyoko mjini Lusaka, Zambia, Herrick Mpuku amesema, mtazamo huo ni muhimu hususan katika zama za sasa ambapo dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa na vita. Katibu mkuu wa Shirikisho la Urafiki kati ya Zambia na China, Fredrick Mutesa amesema, changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kama mabadiliko ya tabianchi na magonjwa ya mlipuko zinahitaji juhudi za pamoja za nchi zote.

Kwa upande wake, Balozi mdogo wa China nchini Zambia, Wang Sheng amesema China imedumu kuwa nguvu kubwa ya amani, utulivu na maendeleo katika dunia inayokabiliwa na mabadiliko makubwa, na kwamba, wakati ikitafuta maendeleo yake, China inafanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia, na pendekezo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja linatoa jibu la China kuhusu aina ya dunia inayotakiwa katika zama za sasa.