Wizara ya Afya ya Ethiopia imetangaza mpango mpya wa kimkakati wa kukinga na kudhibiti virusi vya UKIMWI, ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo Jumatano imesema, katika miaka minne ijayo, Ethiopia itafanya juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya UKIMWI, na kupunguza kiwango cha maambukizi mapya na vifo. Mpango huo unalenga kupunguza kiwango cha kuambukizwa kwa UKIMWI hadi mtu asiyezidi mmoja kati ya watu elfu 10 nchini humo.
Zaidi ya hayo, mafunzo ya kina yanatolewa kwa wadau wote wa mpango huo, ikiwa ni pamoja na wajumbe kutoka sehemu 300 zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIWMI.