UM na washirika wake waunga mkono hatua za serikali ya Madagascar kukabiliana na Kimbunga Gamane
2024-04-05 09:45:07| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Bw. Stephane Dujarric amesema Umoja huo na washirika wake wa kibinadamu nchini Madagascar wanaunga mkono hatua ya serikali ya nchi hiyo kukabiliana na kimbunga Gamane, ambacho kimesababisha nchi hiyo kutangaza kuingia katika hali ya hatari.

Amesema kimbunga hicho cha kitropiki kilichoukumba mkoa wa Sava kaskazini mashariki mwa nchi hiyo Machi 27, kimesababisha vifo vya watu 19, wengine watatu kujeruhiwa na wengine elfu 22 kulazimika kuhama makazi yao.

Washirika wa kibinadamu wanaomba rasilimali zaidi kusaidia juhudi za uokoaji na kuwasaidia wafanyakazi wa misaada kufikia maeneo yaliyoathirika kupitia usafiri wa anga au baharini, kwa kuwa barabara na madaraja yameharibiwa na kimbunga hicho.