Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia vyafikia 60
2024-04-08 22:51:52| cri

Watu 60 wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia katika miezi mitatu iliyopita, ikiashiria hali mbaya ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema katika ripoti yake ya hivi karibuni iliyotolewa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, kwamba kumekuwa na ongezeko dhahiri la kesi za kipindupindu katika miezi mitatu iliyopita, huku kukiwa na jumla ya kesi mpya 4,956 na vifo 60 vikiripotiwa.

Ripoti hiyo imesema, kati ya kesi hizo, kesi 2,503 ni za wanawake, ikisisitiza hatari kubwa ya ugonjwa huo kwa wanawake.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya kesi zilizoripotiwa mwaka huu ni ya juu zaidi kwa mara tatu kuliko ile iliyoripotiwa kwenye kipindi kama hicho katika miaka mitatu iliyopita.