Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat Jumamosi amemteua Adama Dieng wa Senegal kuwa mjumbe maalum wa kwanza wa Umoja huo wa kuzuia uhalifu wa mauaji ya kimbari na ukatili mwingine mkubwa.
Akiwa mjumbe maalum wa kwanza wa Umoja wa Afrika kwenye jukumu hilo, Dieng ataongoza ajenda ya Umoja huo ya kupambana na itikadi ya chuki na mauaji ya kimbari katika bara la Afrika.
Uteuzi wa Dieng unakuja wakati Umoja wa Afrika ukifanya hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi yalipotokea nchini Rwanda.