Makamu wa rais wa Tanzania awataka viongozi wanawake kukabiliana na changamoto za afya duniani
2024-04-08 13:52:28| cri

Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango, amewataka wanawake viongozi kutoka dunia ya kusini kutambua changamoto zao na kubadilishana maoni kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto za kiafya duniani.

Dkt. Mpango amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Afya wa kimataifa wa WomenLift uliofanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania, na kuhudhuriwa na wajumbe 800 kutoka nchi 41 duniani.

Amesema wanawake wanachukua asilimia kubwa ya nguvukazi katika sekta ya afya, ambapo ripoti ya dunia inakadiria kuwa ni asilimia 25 tu ya wahudumu waandamizi na asilimia 5 ya nafasi za juu zinashikiliwa na wanawake.

Kutokana na hilo, Dkt. Mpango ametoa wito kwa wanawake viongozi katika dunia ya kusini kutumia jukwaa hilo kutambua changamoto zao na kubadilishana mawazo ya jinsi WomenLift inavyoweza kusaidia kukabiliana na changamoto hizo.