Ethiopia yadhamiria kuwa kiongozi wa kikanda wa makampuni yanayoibuka
2024-04-08 08:49:13| CRI

Serikali ya Ethiopia imetangaza matarajio yake ya kuwa kiongozi wa kikanda kwa makampuni yanayoibuka haswa katika sekta ya uvumbuzi.

Shirika la Habari la Ethiopia (ENA) limeripoti kuwa, Waziri wa Kazi na Ujuzi wa nchi hiyo Muferihat Kamil amesisitiza msimamo wa serikali wa kuunga mkono makampuni hayo, na haja ya kuongeza ushirikiano kati ya taasisi za serikali, sekta binafsi pamoja na wenzi wa kimataifa katika kuyakuza makampuni hayo.

Waziri wa Viwanda wa nchi hiyo Melaku Alebel pia amesisitiza umuhimu wa kimkakati wa makampuni yanayoibuka, haswa yale ya sekta ya teknolojia, akisema yatachochea maendeleo ya sekta nyingine.  

Kwa mujibu wa Wizara ya Uvumbuzi na Teknolojia ya Ethiopia, nchi hiyo imeshuhudia “ongezeko la kasi” la idadi ya makampuni yanayoibuka katika miaka mitano iliyopita.