Zimbabwe yawa nchi ya tatu Kusini mwa Afrika kutangaza hali ya hatari ya ukame
2024-04-09 08:43:34| cri

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu athari za ukame katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika, na kusababisha Zimbabwe kuwa nchi ya tatu katika kanda hiyo kutangaza hali ya hatari, baada ya Zambia na Malawi kutangaza hali ya hatari kutokana na hali ya hewa ya El Nino.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, zaidi ya watu milioni 2.7 nchini Zimbabwe wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na ukame, licha ya serikali na washirika wa kibinadamu kuwekeza katika mipango inayolenga kumaliza athari mbaya zaidi za ukame.

Kanda ya kusini mashariki mwa Afrika inakabiliwa na hali mbaya ya ukame katika miezi hii kutokana na kuongezeka kwa joto la dunia linalosababisha joto kali katika eneo la mashariki mwa Bahari ya Pasifiki na hali ya hewa ya El Nino.