China ni nguvu chanya kwa uchumi wa Kenya
2024-04-09 08:43:54| CRI

Mwenyekiti wa Muungano wa Makampuni Madogo na ya Kati (MSME) nchini Kenya Ben Mutahi amesema, China ni nguvu chanya kwa uchumi wa Kenya.

Mutahi amesema, China imekuwa chanzo kinachopendelewa zaidi kwa uagizaji wa bidhaa za kielektroniki, nguo, vipodozi, vifaa vya magari na mashine, na kwamba bidhaa za China zinatawala soko la Kenya kwani wateja wanazipendelea kutokana na kuwa zinakidhi mahitaji yao na pia zina bei nafuu.

Kwa mujibu wa Mutahi, viwanda vya China vinaweza kutengeneza idadi kubwa ya bidhaa kwa vipimo vya Kenya kwa siku 30, ikilinganishwa na nchi nyingine, ambazo kwa kawaida huchukua zaidi ya siku 60.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya, thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka China imefikia dola za kimarekani bilioni 3.48 katika mwaka 2022, ikiwa ni asilimia 18.2 ya thamani ya jumla ya uagizaji wa bidhaa ya Kenya kwa mwaka huo.