Marais wa China na Micronesia wafanya mazungumzo
2024-04-09 21:11:17| CRI

Rais Xi Jinping wa China tarehe 9 Aprili mjini Beijing amefanya mazungumzo na rais wa Micronesia Wesley W. Simina ambaye yupo ziarani nchini China.

Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesema mwaka huu ni miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Micronesia. Amesema pande hizo mbili zinatakiwa kudumisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati katika pande zote, kushikilia msingi wa ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, kuharakisha ushirikiano katika kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuimarisha ushirikiano wa miradi wa miundo mbinu na kukuza mawasiliano katika sekta za utamaduni, afya na elimu.

Kwa upande wake rais Simina amesema ushirikiano wa China na nchi za visiwa vya Bahari ya Pasifiki unachangia amani na maendeleo ya kanda hiyo, na kwamba Micronesia itaendelea kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za eneo hilo na China.