Rwanda kuwa mwenyeji wa mkutano wa shirikisho la wasanifu majengo la Jumuiya ya Madola
2024-04-09 10:56:34| cri

Rwanda itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Wasanifu Majengo la Jumuiya ya Madola utakaofanyika kuanzia Agosti 21 hadi 23 mwaka huu, ambao utajadili ajenda mbalimbali zikiwemo uvumbuzi, miji endelevu na jinsi ya kutimiza mahitaji ya ziada ya jamii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano huo, Alex Ndibwami amesema, moja ya lengo kuu la mkutano huo ni kuonyesha uelewa na uvumbuzi unaoibuka sambamba na kusisitiza ujuzi unaohitajika, hususan katika maeneo ya ujenzi wa miji endelevu na uelewa kuhusu hali ya hewa.

Amesema Taasisi ya Wasanifu Majengo ya Rwanda na wenzi wake wanauchukulia mkutano huo kama fursa kubwa ya kutafakari na kuonyesha juhudi katika kuendeleza miji endelevu, ikiwa ni jibu la wito uliotolewa na Mkutano wa Wakuu wa Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika miaka miwili iliyopita.