Afrika kutumia teknolojia ya anga za juu kusaidia maendeleo yake
2024-04-09 08:45:29| CRI

Kamishna wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi wa Umoja wa Afrika, Mohammed Belhocine amesema, Afrika inakaribia kuanzisha Mamlaka ya Anga za Juu ya Afrika (AfSA) kwa lengo la kutumia teknolojia ya anga ya juu kusaidia maendeleo ya bara hilo.

Amesema sera ya Umoja wa Afrika inapendekeza kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo, na hatua zimechukuliwa katika mwaka uliopita na mwaka huu kuhakikisha kuwa Mamlaka hiyo inaanzishwa.

Ameweka wazi kuwa, maandalizi ya kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo ambayo makao yake makuu yatakuwa jijini Cairo, Misri, yametimia kwa asilimia 90, na kwamba mfumo wa uongozi wake umeridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.

Amesisitiza kuwa, kanuni ya msingi ya sera ya anga za juu ya Afrika ni matumizi ya amani ya rasilimali za anga ya juu.