Baraza la Usalama la UM laanza majadiliano juu ya ombi la Palestina kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa
2024-04-09 22:52:56| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeiwasilisha ombi la Palestina kuwa mwanachama rasmi wa Umoja huo kwa Kamati ya Uanachama Mpya ya Baraza hilo, ambapo kwa mujibu wa ratiba, Kamati hiyo itafanya mazungumzo ya ndani kwa mara ya kwanza siku hiyo hiyo.

Palestina kwa sasa ni mwangalizi wa Umoja wa Mataifa na ikitaka kuwa mwanachama rasmi wa Umoja huo, inahitaji idhini kutoka kwa Baraza la Usalama na Baraza Kuu la umoja huo.

Mwaka 2011, rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliwasilisha ombi hilo, lakini Marekani ilisema ni lazima makubaliano yafikiwe kwanza kati ya Palestina na Israel, na kuonya kuwa itatumia haki yake ya kura turufu katika Baraza la Usalama, hivyo kuilazimisha Palestina kusitisha ombi lake