Uchunguzi wa China kuhusu pombe ya brandy inayotoka Umoja wa Ulaya haulengi nchi yoyote ya Umoja huo
2024-04-09 10:57:05| cri

Waziri wa Biashara wa China, Wang Wengtao amesema, uchunguzi unaofanywa na kitengo cha cha China cha kupambana na vitendo vya kuvuruga soko kwa bei ya chini isio ya kawaida kuhusu pombe kali aina ya brandy kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kutokana na malalamiko yaliyotolewa na sekta ya utengenezaji wa pombe ya brandy nchini China, haulengi nchi yoyote mwanachama wa Umoja huo wala hauna matokeo yaliyoandaliwa awali.

Waziri Wang amesema, China itafanya uchunguzi wa wazi usio na kificho kuendana na sheria za China na kanuni za Shirika la Biashara Duniani (WTO), huku ikilinda kikamilifu haki za wadau wote.

Wang amesema hayo alipokutana na ujumbe wa mashirikisho matatu ya wafanyabiashara wa pombe ya brandy  kutoka Ufaransa na watengenezaji watano wa pombe ya brandy kutoka nchini humo, ambao walisema wako tayari kushirikiana na China katika mchakato wa uchunguzi na kuendeleza biashara zao katika soko la China.