Wataalamu wa Afrika wakutana nchini Kenya kuweka maeneo ya kipaumbele katika malengo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2024-04-10 08:29:38| CRI

Wataalamu wa Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kuweka sawa vipaumbele vyao na malengo ya kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mwezi Juni nchini Ujerumani.

Mkutano huo wa siku nne uliowaleta pamoja watunga sera, wadau, mashirika ya wakulima na mashirika ya kijamii kutoka nchi 30 za Afrika, utatoa msimamo wa pamoja wa Afrika kabla ya kikao cha 60 cha Kitengo cha Ushauri wa Kisayansi na Kiteknolojia na Kitengo cha Utekelezaji kitakachofanyika Juni 3 hadi 13 mjini Bonn.

Mkutano huo unatarajiwa kuwapa wahamsishaji wa Afrika mkakati na mtazamo ili kushiriki katika majadiliano kuhusu kilimo, hasara na uharibifu, na fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.