Rais Xi Jinping akutana na aliyekuwa kiongozi wa Taiwan Bw. Ma Ying-jeou mjini Beijing
2024-04-10 23:03:47| cri

Rais Xi Jinping wa China amekutana na aliyekuwa kiongozi wa Taiwan Ma Ying-jeou ambaye yuko mjini Beijing

Kwenye mkutano wao Rais Xi amesema watu kutoka pande zote za mlango bahari wa Taiwan ni wa taifa moja la China, na historia ya zaidi ya miaka 5,000 ya taifa la China imeshuhudia vizazi vilivyofuatana vya mababu wakihamia na kukaa kisiwani Taiwan na watu kutoka pande mbili za Mlango wa Bahari walipambana bega kwa bega ili kuokoa kisiwa kutoka kwa wavamizi wa kigeni.

Rais Xi amesisitiza kuwa watu wa pande zote za mlango bahari wa Taiwan wote ni wachina, na hakuna changamoto ambayo hayawezi kutatuliwa, hakuna masuala ambayo hayawezi kujadiliwa, na hakuna nguvu inayoweza kuwatenganisha. Pia amesema umbali wa mlango bahari wa Taiwan hauwezi kutenganisha uhusiano wa kindugu kati ya watu wa ng'ambo mbili za mlango bahari huo.

Amesema tofauti katika mifumo haibadilishi ukweli kwamba pande zote mbili za mlango Bahari ni za China moja, na kuingiliwa na nje hakuwezi kurudisha nyuma mwelekeo wa kihistoria wa kuunganisha tena taifa.