Huawei yatoa mafunzo kwa roboti katika maonyesho ya wanafunzi nchini Kenya
2024-04-10 08:28:35| CRI

Kampuni ya Huawei ya China jana imetangaza kuwa, darasa la kidijitali linaloitwa DigiTruck linalotoa mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kwa jamii zilizo msikini barani Afrika, litatoa mafunzo ya papo kwa hapo kwa njia ya roboti katika toleo la 60 la Maonyesho ya Sayansi na Ufundi ya Kenya yaliyoanza jana.

Kampuni hiyo imesema, wanafunzi wa shule za sekondari wanatarajiwa kupata fursa ya kujifunza na kushiriki mafunzo hayo kama sehemu ya shughuli hiyo ya wiki nzima.

Katika taarifa yake iliyotolea jijini Nairobi, kampuni hiyo imesema inafurahi kuwa sehemu ya shughuli hiyo, ambayo inaendana na ahadi yake ya kuboresha fursa za mafunzo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya.

Maonyesho ya Sayansi na Ufundi ya Kenya ni tukio la kila mwaka linalotumika kuonyesha miradi ya ubunifu na mawazo ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini humo.