Waziri Mkuu Li Qiang ampongeza Bi. Judith Tuluka kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa DRC
2024-04-10 11:07:44| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang ameongea kwa njia ya simu na Bi. Judith Suminwa Tuluka, na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Bw. Li Qiang amesema, China na DRC ni wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uongozi wa rais Xi Jinping wa China na rais Felix Tshisekedi wa DRC, urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili unazidi kuimarika, huku ushirikiano na mawasiliano katika sekta mbalimbali yakiongezeka.

Bw. Li amesema serikali ya China inatilia maanani uhusiano kati ya China na DRC, na anapenda kufanya juhudi pamoja na Bi. Tuluka na serikali ya awamu mpya ya nchi hiyo kutekeleza vizuri makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais hao wawili, kushikilia kuungana mikono katika maslahi makuu ya upande mwingine, na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili wenye ufanisi, ili kuyafanya matunda ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na DRC yawanufaishe zaidi watu wa nchi hizo mbili.