Rais wa Kenya azitaka taasisi za kidini kushirikiana na serikali kukabiliana na maovu katika jamii
2024-04-10 11:04:53| cri

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali na mashirika ya kidini yana jukumu la pamoja kushirikiana kwenye juhudi za kukabiliana na maovu katika jamii na kuziinua kiuchumi.

Akizungumza jana wakati wa Kikao cha 24 cha Baraza Kuu la Kanisa la PCEA, jijini Nairobi, Rais Ruto amesema serikali itaendelea kushirikiana na makanisa ili kuboresha kiwango cha maisha cha Wakenya. Pia ameeleza kuridhishwa kwake na jukumu linalotekelezwa na makanisa katika kuendeleza elimu, afya kati ya masuala mengine muhimu.

Rais Ruto amewaomba viongozi wa dini kuisaidia serikali kukabili pombe haramu, matumizi ya mihadarati na changamoto za ukosefu wa usalama zinazotokana na wizi wa mifugo.