Watu 38 wafariki baada ya boti ya wahamiaji kupinduka katika pwani ya Djibouti
2024-04-10 08:29:46| cri

Ubalozi wa Ethiopia nchini Djibouti umesema, watu 38 wamefariki wakiwemo watoto na watu wengine sita hawajulikani walipo baada ya mashua iliyobeba wahamiaji wa Ethiopia kupinduka katika pwani ya Djibouti jumatatu wiki hii.

Katika taarifa yake, Ubalozi huo pia umesema meli hiyo ilikuwa imebeba wahamiaji 60 wa Ethiopia waliokuwa wakielekea Yemen wakati ajali hiyo ilipotokea.